134

Tafuta Daima Utakatifu

1

Tafuta daima utakatifu, fanya urafiki na watu wote, Nena siku zote na Bwana wako, baraka uombe kwa kila jambo.

2

Tafuta daima utakatifu, uwe peke yako ukimwabudu, Ukimwangalia Mwokozi wako, utabadilishwa kama alivyo.

3

Tafuta daima utakatifu, kiongozi wako awe Yesu tu, Katika furaha au huzuni, dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

4

Tafuta daima utakatifu, umtawaze roho moyoni mwako, Akikuongoza katika haki, hufanywa tayari kwa kazi yake.