1
Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi, Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu, Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona, Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.
2
Saa heri ya maombi, twapeleka dhiki zetu, Kwake aliyeahidi, kubariki wenye haja, Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake, Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.
3
Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia, Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo, Yesu atatusikia, tutamtafuta daima, Na tutakapokutana, tutamwona-saa tamu.