1
Nitakuandama kote, nitakapoangizwa. Wewe ukiniongoza, nami nitaandama.
Kiitikio
Nitakuandama kote, naam ulinifia, Kwa neema yako Bwana, napenda kuandama.
2
Njia ijapoparuza, kwa miiba na fujo, Ulitangulia mbele, nami nitaandama.
3
Nijapokuta taabu, na majaribu kote, Nakumbuka shida yako, nami nitaandama.
4
Nijapoona ukiwa, na mateso makali, Wewe uliyatikiza, nami nitaandama.
5
Ijapo wanipeleka, vilindini mwa giza, Wewe uliyatikiza, nami nitaandama.