1
Uliniimbie tena, neno la uzima, Uzuri wake nione, neno la uzima, Neno hili zuri, lafundisha kweli.
Kiitikio
Maneno ya, uzima ni, maneno mazuri, Maneno ya, uzima ni, maneno mazuri.
2
Kristo anatupa sote, neno la uzima, Mwenye dhambi asikie, neno la uzima, Latolewa bure, tupate wokovu.
3
Neno tamu la injili, neno la uzima, Lina amani kwa wote, neno la uzima, Litatutakasa, kwa haki ya mwana.