1
Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu sasa, naja.
2
Hivi nilivyo si langu, kujiosha roho yangu, Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu sasa, naja.
3
Hivi nilivyo sioni, kamwe furaha moyoni, Daima ni mashakani, Bwana Yesu sasa, naja.
4
Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu, Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu sasa, naja.
5
Hivi nilivyo mimi tu, siwezi kujiokoa, Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu sasa, naja.
6
Hivi nilivyo, mapenzi yamenipa njia wazi, Hali na mali sisazi, Bwana Yesu sasa, naja.