141

Chini ya Msalaba

1

Chini ya msalaba, nataka simama, Ndio mwamba safarini, wa kivuli chema, Ni kweli kwa roho yangu, ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu, wakati wa hari.

2

Hapa ni pema sana, ni ngome kamili, Hapa yameonekana, mapenzi ya kweli, Kama alivyoonyeshwa, Yakobo zamani, Msalaba umekuwa, ngazi ya mbinguni.

3

Na Yesu Msalabani, walimkemea, Alikufa niokoke, niliyepotea, Naona ajabu sana, ya mambo mawili, Jinsi alivyonipenda, nisiyestahili.

4

Atakayeonana na, Yesu mbinguni, Njia yake aanzapo, ni Msalabani; Wokovu upo hapa tu, mwingine hapana, Kisha kuna furaha kuu, pamoja na Bwana.