1
Nasikia mwito, ni sauti yako, Nikasafiwe kwa damu, ya kwangikwa kwako.
Kiitikio
Nimesogea, mtini pako, Unisafi kwa damu, ya kuangikwa kwako.
2
Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu, Ulivyonisafi taka, ni utimilivu.
3
Yesu hunijuvya, mapenzi imani, Tumai amani radhi, hapa na mbinguni.
4
Napata wokovu, wema na neema, Kwako Bwana nina nguvu, na haki daima.