1
Baba sina msaada ila kwako pekee, Kama kwangu ungefichwa, nifanyeje Baba?
Kiitikio
Sasa hivi naamini, Yesu alikufa, Aliimwaga damu yake, nitoke dhambini.
2
Naamini mwana wako, nipe nguvu zako, Nijazie mahitaji, katika saa hii.
3
Ni furaha gani kwangu, kukuona uso, Nijue sauti yako, nipate neema.