144

Ni Wako Bwana

1

Ni wako Bwana, ninasikia, unaponena nami, Lakini kweli, nataka kwako, nizidi kusogea.

Kiitikio

Bwana vuta, (vuta) nije nisongee, Sana kwako mtini, Bwana vuta, (vuta) nije nisogee, Pa damu ya thamani.

2

Niweke sasa, nikatumike, kwa nguvu za neema, Uyapendayo, nami nipende, nizidi kukwandama.

3

Nina furaha, tele kila saa, nizungumzapo nawe, Ninanena kama kwa rafiki, nikipiga magoti.