1
Twae wangu uzima, sadaka ya daima, Twae saa na usiku, zikutukuze huku.
2
Twae mikono nayo, ifanye upendayo, Twae yangu miguu, kwa uongozi wako tu.
3
Twae sauti yangu, niimbe kwa Mungu tu, Itwae na midomo, ijae neno lako.
4
Twae dhahabu pia, na yote ya dunia, Twae yangu hekima, upendavyo tumia.
5
Nia itwae Mungu, haitakuwa yangu, Twae moyo ni wako, uwe makazi yako.
6
Twae mapenzi yangu, sifa za moyo wangu, Twae kabisa nafsi, niwe wako halisi