147

Tawala Ndani Yangu

1

Tawala ndani yangu, ee Yesu mfalme, Uwe kwangu majibu, kwa maswali yangu, Uishi ndani yangu, wewe mwongozi, Utumishi ni wangu, wako utukufu.

2

Hekalu nimetoa, umelisafisha, Sasa fahari yako, imulike ndani, Dunia iwe kimya, mwili sasa uwe, Mtumwa mtulivu, wa kukutii tu.

3

Viungo vyake mwili, vyote vyakungoja, Tayari vikiitwa, kwenda kusimama, Bila manung’uniko, au malaumu, Au kusumbuliwa, pasipo majuto.

4

Niwe na utulivu, pasipo haraka, Tayari kungojea, maagizo yako, Tawala ndani yangu, ee Yesu mfalme, Uwe kwangu majibu, kwa maswali yote.