1
Univute karibu Baba, unikumbatie, Unisogeze kifuani, nataka pumziko.
Kiitikio
Univute karibu, (Vuta univute karibu) Kwa kamba za upendo, (Kwa kamba, kamba za upendo) Univute (Kwa kamba za upendo, univute karibu) Karibu nawe. (Univute karibu)
2
Univute Mwokozi wangu, na tusiachane, Mikono yako juu, yangu leo niione.
3
Univute kwa roho yako, nifanane nawe, Unioshe unihuishe, niwe safi huru.