149

Kuwa Wake Yesu

1

Kuwa wake Yesu, je ni kusudi lako? Ungeenda naye, njia nyembamba? Unataka aubebe, mzigo wako? Awe Mwongozi wako.

Kiitikio

Uwezo wake unakutosha, na damu yake itakusafi, Kwa vile ukubali ni bora, afanye mapenzi yake nawe.

2

Unataka kuitika, anapokwita? Kupata amani, kwa kumpa vyote? Wataka uwezo, usianguke kamwe? Awe Mwongozi wako.

3

Wataka raha katika, ufalme wake? Ungeshinda kwa majaribu yote? Ungefanya kazi yake, vizuri sana? Awe Mwongozi wako.