154

Yanipasa Kuwa Naye

1

Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu, Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.

Kiitikio

Moyo hauogopi, wala kutikisika. Nitakwenda apendapo, kwa kuwa anilinda.

2

Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea, Anaweza kufariji, na maneno matamu.

3

Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote, Yakiwapo majaribu, na mashaka yo yote.

4

Yanipasa kuwa naye, katika njia zangu, Macho yake yaongoza, hatua zangu zote.