1
Njiani huniongoza, Yesu wangu Mwokozi, Rehema hatapunguza, milele kiongozi, Ina raha kwandamana, duniani daima, Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema.
2
Njiani huniongoza, hupunguza matata, Nikiugua hupoza, na njaa ninashiba, Lichokapo guu langu, nguvu zikapungua, Jiwe lilo mbele yangu, hunibubujikia.
3
Njiani huiongoza, kwa pendo lililo kuu, Mwisho atanituliza, kwake Baba yangu juu, Nikivikwa kutokufa, nikae na Mwokozi, Nitamsifu sana sifa, kweli ni kiongozi.