1
Uniongoze Yehova, ni msafiri chini, Ni mnyonge u hodari, nilinde kwa mkono. Unitunze, unilinde, unionyeshe njia.
2
Na kisima cha uzima, maji ya utabibu, Fungua na moyo wangu, ninywe na kuponyeka, Uninyweshe, unilishe, hata nimetosheka.
3
Wakati wa kuuvuka, ule mto Yordani, Hofu yangu hufariji, nione uso wako, Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, nitaimba daima.