1
Mfalme yu mlangoni, ndiye aliyetufia, Mara wote wampendao, atawakusanya.
Kiitikio
Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama, Anakuja, anakuja, kuja kwake karibu.
2
Dalili za kuja kwake, zinazidi kutimizwa, Karibuni wateule, watamlaki Bwana.
3
Sitafute duniani, amani wala furaha, Mpaka Bwana arudi, dhambi kuondoa.
4
Tutakaa na Mwokozi, makaoni ya milele, Daima tutafurahi, kuwa watu wake.