159

Anakuja Upesi

1

Anakuja upesi Yesu Bwana wetu, msafiri mbali na kwao, Alisema dhahiri “Nitakuja tena,” amina na uje Ee Bwana.

Kiitikio

Yuaja, Yesu atarudi sasa, anakuja duniani, Wasafiri wote watapumzika, Yesu anaporudi tena.

2

Makaburi yote wafu wanapolala, yatafunguliwa tena, Na maelfu pale wataondoka tena, wasione machozi kamwe.

3

Hatutatengana na hao tena huko, nyimbo nzuri tutaimba, Watakusanyika toka kila kabila, miguuni pa Mwana Kondoo.

4

Aleluya amin aleluya tena, upendo wake unashinda, Tutamsifu milele hata tutashangaa, jinsi alivyotukomboa.