1
Watakatifu kesheni, nguvu za mbingu zagonga, Washeni taa tayari, kwa kurudi kwake Bwana.
Kiitikio
Yuaja, Yesu mfalme, yuaja mwenye fahari, Yesu yuaja enzini, karibu Yesu uje.
2
Piga mbiu tangazeni, habari ya ukombozi, Ya mponya wa upendo, nayo nguvu ya samaha.
3
Falme nyingi zaangushwa, panda ya saba yalia; Tangaza neema yake, kabla ya kupita saa.
4
Mataifa yapotea, nchi zajaa uchungu, Kristo anaharakisha, unabii unatimizwa.
5
Wenye dhambi njoni sasa, Kristo awapatanishe, Mbio twaeni neema, kitambo muda waisha.