1
Bwana ninakuhitaji, Ni mpofu, maskini, Unishike mkononi, kwako napata nguvu.
Kiitikio
Kila saa, kila saa, Bwana ninakuhitaji, Kila saa, kila saa, unilinde kila saa.
2
Univike na mavazi, ya usikivu wako, Nguo zangu zote chafu, nazitamani zako.
3
Wewe ukiniongoza, nitakwenda salama, Nenda nami siku zote, u nuru na uzima.
4
Na ikiwa huko mbele, sehemu yangu ngumu, Au ikiwa furaha, unilinde kila saa.