161

Piga Panda

1

Piga panda na ya makelele, Yesu yuaja tena, Ipaze sauti imba sana, Yesu yuaja tena.

Kiitikio

Anakuja, anakuja, Yesu yuaja tena.

2

Itoe mwangwi sana vilima, Yesu yuaja tena, Yuaja kwa utukufu mwingi, Yesu yuaja tena.

3

Itangazwe mahali po pote, Yesu yuaja tena. Mwokozi aliyetufilia, Yesu yuaja tena.

4

Kuona machafuko twajua, Yesu yuaja tena, Mataifa yakasiriana, Yesu yuaja tena.

5

Maradhi hofu hutuhubiri, Yesu yuaja tena. Taabu, njaa hutulilia, Yesu yuaja tena.