1
Pengine ni saa ya kupambazuka, mishale ya jua ipenyapo giza, kwamba atakuja Yesu mtukufu, awapokee wake.
Kiitikio
Bwana itakuwa lini, tutakapoimba, “Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin, Aleluya, Amin?”
2
Pengine mchana pengine jioni, pengine usiku wa manane, giza litatoweka kwa fahari akija, awapokee wake.
3
Majeshi yake yataimba ‘hosana,’ na watakatifu waliotukuzwa, watamsifu kwa kuwa amekuja, awapokee wake.
4
Furaha tukiitwa pasipo kufa, pasipo kuona maradhi machozi, kuchukuliwa winguni kwa fahari, akija kwa watu wake.