164

Unakaribia Wakati

1

Unakaribia wakati wa kuja kwa Yesu, Atawachukua watu wake nyumbani juu.

Kiitikio

Tunaiona mishale ya nuru inayopenya giza, Tunaiona mishale ya nuru ya ufufuo.

2

Injili inatangazwa pote kwa mataifa, Bwana wa Arusi atakuja na tarumbeta.

3

Pamoja na malaika zake Bwana arudi, Awapeleke waaminifu wasife tena.

4

Wapenzi waliotengwa kale watakutana, Machozi yao wenye huzuni yatafutika.