165

Ahadi Tamu

1

Ahadi tamu kwa waamini, tazama nakuja upesi sana, Uwe imara hatari kubwa, ndugu usilale, bali ukeshe.

Kiitikio

Uihifadhi imani yako, dunia mpya itatolewa. Njoo ingia furaha yangu, taji zinangoja, uwe imara.

2

Tutakesha na kutoa sala, atakuja kama mwivi kwa wengi, Ya kwamba yu karibu twajua, ila hatujui ni siku gani.

3

Tunategemea neno lake, ambalo latangaza kuja kwake, Tumaini letu ni ahadi, “naja karibuni,” uwe imara.