1
Yesu Bwana Mwokozi, aishi milele, Najua kwamba yupo, pamoja na mimi; Sauti nasikia, rehema naona, Wakati namhitaji, yupo nami.
Kiitikio
Yu hai, yu hai, yu hai Bwana Yesu, Atembea, azungumza nami siku zote. Yu hai, yu hai, kutoa uzima, Hivi ndivyo nijuavyo, Yu hai ndani yangu.
2
Ulinzi wake upo, naona dhahiri, Miguu ichokapo, sikati tamaa, Najua aniongoza, katika dhoruba, Siku ya kuja kwake, nitamwona.