1
Tarumbeta ya Mwana itakapolia mara, Milele itakapopambazuka, Nao wa haki watakapokusanyika ng’ambo, Majina yaitwapo lo! niweko.
Kiitikio
Majina yaitwapo lo, Majina yaitwapo lo, Majina yaitwapo lo, Majina yaitwapo lo niweko.
2
Siku ile watakatifu watakapoamka, Nakuondoka huru kaburini, Watakapokusanyika makaoni kule juu, Majina yaitwapo lo niweko.
3
Tutende kazi ya Yesu mchana kutwa kwa bidii, Tutangaze kote pendo lake kuu, Nayo kazi itakapotimika hapa chini, Majina yaitwapo lo niweko.