169

Hapo Yesu Atakapoita

1

Hapo Yesu atakapoita, mataifa mbele yake, Tutashindaje kwenye hukumu, mbele ya kiti cha enzi.

Kiitikio

Atakusanya ngano ghalani, atatupa mbali makapi, Tutashindaje hukumuni, siku kuu ya kiyama?

2

Je tutasikia neno tamu, “Vema wewe mtumwa mwema,” Ama wenye uchungu na hofu, tutakatazwa ufalme?

3

Atakubali tu kwa furaha, watoto wake wapendwa, Atawapa mavazi meupe, wakae kitini pake.

4

Hivyo tukeshe nasi tungoje, wenye taa zinazowaka, Tutakapoitwa arusini, tuwe tayari kumlaki.

5

Roho ikielekea mbingu, twangoja wenye saburi, Hata safari yetu iishe, tukae kwake milele.