1
Siitafuti mali, wala utajiri, Nataka kwa yakini, nipate Mwokozi. Chuoni mwa ufalme, niambie Yesu, Jina langu yakini, je limeandikwa?
Kiitikio
Je limeandikwa? Jina langu huko? Kitabuni mbinguni, je, limeandikwa?
2
Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga, Lakini damu yako, mwokozi yatosha, Kwani umeahidi, zijapo nyekundu, Zitakuwa nyeupe, ilivyo theluji.
3
Mji mzuri sana, wa majumba makuu, Walipo malaika, mji bila ovu, Wakaapo walio, na mavazi safi, Je limeandikwa, jina langu huko.