1
Imeanzishwa hukumu mbinguni, tutasimamaje pale, Apimapo Mungu Hakimu, kila wazo na tendo?
Kiitikio
Tutasimamaje sote katika siku kuu ile? Dhambi zetu zitafutika, ama zitatuangusha?
2
Wametangulia wafu kupimwa, kitambo ndipo wahai, Watapokea neno la mwisho, vitabuni mwa Mungu.
3
Tutasimamaje usiku ule, siri zetu kila moja, Zafunuliwa toka vitabu, Yesu atusaidie!