1
Mfalme wetu atuita, tukae karamuni kwake, Itakuwaje nasi kule, Bwana ajapo?
Kiitikio
Bwana ajapo ndugu, Bwana ajapo, Itakuwaje na sisi, Bwana akija?
2
Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba, Kweli tukeo la fahari, Bwana ajapo.
3
Kwa furaha awakubali, wenye mavazi ya arusi, Tu wa heri tukimridhisha, Bwana ajapo.
4
Kutakuwako na utengo, watalia waliomwasi, Cha kutisha kipindi kile, Kristo ajapo!
5
Mfalme utupe neema, sisi tunapokungojea, Tusiogope kukuona, ujapo Bwana.