173

Hatujui Saa

1

Hatujui saa ya kuja kwa Bwana, lakini dalili zasema karibu, Atakaporudi lakini kwa kweli, hatujui saa.

Kiitikio

Atakuja, kwa vile tukeshe, Atakuja, Mwokozi aleluya, Atakuja kwa fahari, ya baba yake, Hatujui saa.

2

Pana nuru kwao wapendao haki, pana kweli katika chuo cha Mungu, Unabii hufundisha kuja kwake, hatujui saa.

3

Tutakesha na tutaomba daima, tutafanya kazi mpaka akija, Tutaimba na tutasoma ishara, hatujui saa.