174

Sijui Atakapokuja

1

Sijui atakapokuja, mchana au usiku, Labda saa ya alasiri, pengine ni alfajiri, Hutwambia tuwe tayari, taa zetu tusizime, Ili ajapo atukute, tuwe tukimngoja Yeye.

Kiitikio

Tu... kimngoje.......a, (Kukesha tunakungoja Wewe) Tu... kimngoja.......a, (Kukesha tunakungoja Wewe) Tu... kimngoje........a, (Kukesha tunakungoja wewe) Twakesha twamngoja Yeye.

2

Nakumbuka huruma zake, bei ya wokovu wetu, Aliacha nyumba tukufu, awafilie wabaya, Ninadhani itampendeza, kama sisi watu wake, Tukionyesha pendo letu, tuwe tukimngoja Yeye.

3

Ee Yesu Mwokozi mpendwa, wajua nalihifadhi, Tumaini la kukuona, la kukaribishwa nawe, Ukija kwa watu wengine, kama mhukumu wao, Kwangu utakuwa rafiki, nakesha nakungojea.