175

Nitaonana na Yesu

1

Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli, Siku ile shangwe tele, nikimwona Mwokozi.

Kiitikio

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni, Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

2

Sasa siwezi kujua, jinsi alivyo hasa, Bali atakapokuja, nitamwona halisi.

3

Mbele yake yafukuzwa, machozi na huzuni, Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.

4

Uso kwa uso hakika, palepale furaha, Nitafurahi kabisa, nikimwona Mwokozi.