1
Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu, Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.
Kiitikio
Naam twonane mtoni, watakatifu kwenu ni mtoni, Tutakutanika kule mtoni, penye kiti cha Mungu.
2
Tukitembea mtoni, na Yesu mchunga wetu, Daima tu ibadani, usoni pake kwetu.
3
Tukisafiri mtoni, tutue ulemeao, Wema wa Mungu yakini, una taji na vazi
4
Kwang’ara sana mtoni, cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, tumsifu kwa nyimbo.
5
Karibu sana mtoni, karibu tutawasili, Mara huwa furahani, na amani ya kweli.