1
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka, Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi, nivukapo ng’amboni, Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Kiitikio
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso, Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
2
Kuona uso wake, kutanipa Furaha, Furaha isiyo ya kukomesha, Nitamsifu Mwokozi, kwa rehema na pendo, Vilivyonipa pahali mbinguni.
3
Nao waliokufa, katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu, Lakini nifikapo, kwake huko mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
4
Milangoni mwa mji, Bwana atanipisha, Pasipo machozi wala huzuni, Nitauimba wimbo, wa milele lakini, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.