1
Ukingoni mwa Yordani, ninaangalia, Bara nzuri ya Kanaani, ninayotamani.
Kiitikio
Tutakaa pamoja na Yesu, Katika pwani yenye raha, Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo, Milele hata milele.
2
Bara ile ina nuru, nuru ya milele, Kristo jua hutawala, hufukuza giza.
3
Nitapafikia lini, na kubarikiwa, Penye ufalme wa Baba, na kumwona uso.
4
Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa, Siyaogopi mawimbi katika Yordani.