180

Pana Mahali Pazuri Mno

1

Pana mahali pazuri mno, twapaona kwa mbali sana, Baba yetu angoja pale, amepanga makao yetu.

Kiitikio

Kitambo tu bado, tutakutana ng’ambo pale, Kitambo tu bado, tutakutana ng’ambo pale.

2

Tutaimba pale kwa moyo, nyimbo tamu za wenye heri, Na rohoni hatutaona, tena haja ya kupumzika.

3

Kwa Baba yetu mkarimu, tutatoa shukrani sana, Kwa kipaji cha pendo lake, na baraka anazotupa.