182

Mchana Hauishi

1

Mchana hauishi, mjini mzuri, Mji hautapita, na hapana giza.

Kiitikio

Machozi yatafutwa, kifo hakuna kule, Hawahesabu siku, na hapana giza.

2

Milango ni ya lulu, mjini mzuri, Dhahabu njia zake, na hapana giza.

3

Milango haifungwi, mjini mzuri, Mto ni wa uzima, na hapana giza.

4

Hawahitaji jua, mjini mzuri, Mwana Kondoo nuru, na hapana giza.