184

Vitu Vyote ni Sawa

1

Vitu vyote ni sawa, panapo pendo, Kila sauti tamu, panapo pendo. Pana amani pale, na furaha nyumbani, Siku zote salama, panapo pendo.

Kiitikio

Panapo upendo, siku zote salama, panapo pendo.

2

Furaha i nyumbani, panapo pendo, Hapana machukizo, panapo pendo, Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi, Maisha ni kamili, panapo pendo.

3

Hata mbinguni juu, pana furaha, Wakiona upendo, nyumbani mwetu. Macho yanapendezwa, na viumbe vya Mungu, Naye Mungu huona, panapo pendo.

4

Ee Yesu niwe wako, wako kabisa, Ndipo patakuwako pendo nyumbani. Nitakaa salama, sitaifanya dhambi, Nitabarikiwa tu, panapo pendo.