1
Mungu u mapenzi makamilifu, yapitayo fahamu za watu, Twanyenyekea sisi wapungufu, wape baraka wapenzi wetu.
2
Ewe Mapenzi yasiyopimika, twawaombea kitini Mwako, Wape mapenzi yasiyotindika, waliooana mbele yako.
3
Ewe uhai, wewe u dhamana, ya imani na matumaini, Wape kuvumilia hapa sana wasiche maumivu mwishoni.
4
Wape furaha hiyo iwezayo, kutia nuru kwenye huzuni, Wape amani hiyo itokayo, katika matata duniani.
5
Waende mbele kusaidiana, maisha yao ulimwenguni, Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, wafurahi milele mbinguni.