1
Tuonanapo na rafiki sote twafurahi, Ila tumepaswa mwishowe kuagana tena.
Kiitikio
Hatutaagana tena nyumbani mbinguni, Kwenye nchi tamu juu, hatutaagana.
2
Twatumaini kwa furaha tutaonana juu, Na rafiki tulioaga tuishapo shinda.
3
Kule hatutatamka kamwe neno la kuaga, Tutaimba daima tena nyimbo za furaha.