1
Kufariki naye Yesu, usingizi wenye heri, Raha isiyofujika, kwa majonzi na adui.
2
Kufariki naye Yesu, lo ya kubwaga simanzi Na kulala na amani, hata Bwana awatuze.
3
Kufariki naye Yesu, heri watakaoamshwa, Wataona siku ile, utukufu wake Bwana.
4
Kufariki naye Yesu, wataamka aitapo, Watapasua kaburi, na kutoka watukufu.