1
Wimbi la damu ya Yesu, linatutakasa, Aliumia kusudi, tupate uzima.
Kiitikio
Wimbi la damu naona, naingia natakaswa, Bwana asifiwe sana, hutakasa hutakasa.
2
Damu inasema kwangu, nasikia mvuto, Inasema moyo wangu, hutakaswa nayo.
3
Naondoka kutembea, kwa nuru ya mbingu, Mavazi yamesafishwa, moyoni ni Yesu.
4
Neema ni ya ajabu, kutakaswa ndani, Na kuwa naye Yesu tu, aliye Mwokozi.