189

Mimina Upya

1

Mimina upya, nguvu toka juu, Tupe pendo lako, ewe Mwokozi.

Kiitikio

Twakusihi sana, Yesu Mwokozi, Tubatize upya, kwa Roho leo.

2

Kwako twalia, wenye maovu, Osha moyo wetu, ututakase.

3

Kipaji cha juu, kitume kwetu, Tubariki sasa, utufariji.

4

Isikilize, kwa moyo wazi, Sauti ya Roho, ubarikiwe. Meza ya Bwana