190

Raha Yangu Yote, Bwana

1

Raha yangu yote Bwana, i mbavuni pako, Mimi sina haja tena, ila kifo chako.

2

Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu, Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu.

3

Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu, Nioshe damuni mwako, liwe fungu langu.

4

Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo, Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo,

5

Na iwe kafara damu, nifanyapo kazi, Hata imani itimu, nikuone Mwokozi.