19

Msalabani pa Mwokozi

1

Msalabani pa Mwokozi, hapo niliomba upozi, Moyo wangu ulitakaswa, na asifiwe.

Kiitikio

Na asifiwe, na asifiwe, Alinikomboa kwa damu, na asifiwe.

2

Chini ya mti msumbufu, niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, na asifiwe.

3

Kwa ajabu ninaokoka, Yesu anakaa moyoni; Mtini alinifilia, na asifiwe.

4

Damu ya Yesu ya thamani huniokoa makosani, Huniendesha wokovuni, na asifiwe.