20

Mungu Wetu Yeye Mwamba

1

Mungu wetu yeye mwamba, kimbilio taabuni, Msaada penye shida, ulio karibu sana.

Kiitikio

Mwamba wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha, Huongoza katika njia, kimbilio taabuni.

2

Mchana usiku yeye, kimbilio taabuni, Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana.

3

Iwayo yote Yeye tu, kimbilio taabuni, Twamjua Yeye mlinzi, aliye karibu sana.

4

Mungu wetu ficho kwetu, kimbilio taabuni, Siku zote uwe boma, lililo karibu sana.