192

Mwamba Wenye Imara

1

Mwamba wenye imara, kwako nitajificha, Maji hayo na damu, yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi.

2

Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria. Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii, Hayaishi makosa, ndiwe wa kuokoa.

3

Sina cha mkononi, naja msalabani, Nili tupu nivike, ni mnyonge nishike, Nili mchafu naja, nioshe nisijafa.

4

Nikungojapo chini, na kwenda kaburini, Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini, Roho yangu na iwe, rahani mwako wewe.