1
Twaomba Bwana, umpokee kama mhudumu, Ambaye anajitoa, kuwa mtumishi.
2
Twaomba Bwana, umpokee kama mhudumu, Neno lako alitoe, mwangaza kung’aa.
3
Mwokozi wetu, twaomba na umwandikie, Kitabuni mwako, juu mjumbe wa injili.
4
Silaha zake, apewe kumshinda adui, Vitani awe hodari, mpaka mauti.
5
Yeye ashindaye, Bwana kwa rehema yako, Ile taji ya dhahabu, nawe utampa. Kuweka Kanisa Wakfu