1
Msingi wa Kanisa ndiye Yesu Bwana, Kiumbe chake kipya akipenda sana, Kutaka ‘kitafuta alishuka chini, Naye kwa haja yake, akafa mtini.
2
Lina kila kabila kisha ndiyo moja, Wokovu wake una Mwokozi mmoja, Uzazi ni umoja moja tumaini, Chakula ni kimoja, moja tumaini.
3
Watu hustaajabu kwa mashaka yote, Yaipatayo nje hata ndani mwote, Ila watakatifu humwomba wakikesha, Usiku ni kilio, asubuhi raha.
4
Mashaka na taabu hata vita vyake, Vyangoja matimizo ya amani yake, Ndipo kwa macho yetu twone utukufu, Kanisa ya kushinda, itastarehe juu